Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast, Pacome Zouzoua, ameahidi kuipambania Young Africans katika mchezo wa Mzunguuko wa pili wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Ahly.
Kauli kiungo huyo aliyesajiliwa Young Africans msimu huu akitokea Asec Mimosas, imekuja baada ya timu yao kupoteza mchezo wa Mzunguuko wa kwanza wa Kundi D kwa kufungwa mabao 3-0 ugenini dhidi ya CR Belouizdad ya nchini Algeria.
Young Africans itashuka dimbani Jumamosi (Desemba 02), ikipewa matumaini makubwa ya kupambana na kupata ushindi wa kwanza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya Al Ahly.
Pacome amesema wachezaji na Benchi la Ufundi wote wamesahau matokeo yaliyopita dhidi ya CR Belouizdad na badala yake akili na nguvu zao wamezihamishia kwa Al Ahly.
Pacome amesema katika mchezo huo, wanakwenda kushinda na siyo kitu kingine ili kuhakikisha wanajiwekea mazingira ya ushindi hasa mechi za nyumbani, huku akibainisha kwamba, yeye binafsi atahakikisha anatengeneza nafasi za kufunga pamoja na kufunga mwenyewe.
“Kwanza nianze kwa kushukuru kurejea salama nyumbani, na moja kwa moja kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Al Ahly.
“Pili, tunajiandaa kufanya vizuri kuhakikisha tunashinda mechi hii, binafsi nitafanya juhudi kuona nafunga au kutengeneza nafasi ya kufuriga, amesema Pacome.