Uongozi wa Dodoma Jiji, umesema kuwa, umebakiza mechi moja kwa mwezi Novemba, hivyo wanaendelea kufanya maandalizi ili kushinda kwani lengo lao kubwa ni kujiweka nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Moses Mpunga ambaye ni Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, amesema mipango yao kwenye mechi zilizobaki ni kushinda ili wazidi kufikia malengo.

“Tuna kila sababu ya kufika pale tunapopataka kwa sababu wametuzidi alama moja tu na kwa mechi tulizobakiza, hapo tuna uhakika wa kufika bila ubishi iwe kwa mechi ya nyumbani au ugenini.

“Mwalimu anaandaa kikosi chake vizuri kwa ajili ya mashambulizi ya mechi zijazo kwani haitokuwa kinyonge, nawaonea huruma sana tutakaokutana nao maana nawaona kabisa hawatoboi,” amesema Mpunga.

Dodoma Jiji wapo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na alama 15 sawa na Singida Fountain Gate wanaokamata nafasi ya tano, huku wakipishana alama moja na KMC ambao wapo nafasi hiyo ya 4 wakiwa na alama 16.

Tukiondoa tofauti zetu tutafanikiwa - Bwege
Waziri Silaa aikataa dhambi mbele ya Mchungaji