Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungala maarufu kama Bwege, amesema amekuwa na uhusiano na Mbunge wa sasa wa eneo lake Ally Kasinge na kwamba lengo lao ni kuona jimbo hilo linakuwa na maendeleo bila kuangalia tofauti zao za kisiasa, huku akisisitiza kuwa kama chama alichojiunga nacho kwasasa hakitafikia malengo kwa kuwapigania wananchi basi atahamia chama kingine.

Akiongea na Dar24 Media katika mahojiano maalum hivi karibuni, Bwege amesema licha ya kuwa nje ya Bunge lakini changamoto za wakazi wa Kilwa zimekuwa zikitatuliwa kutokana na Rais Dkt. Samia Suluh Hassan kuruhusu kusikilizwa kwa hoja zenye mashiko kutoka kwa wapinzani na kwamba ili kupiga hatua za kimaendeleo ni vyema kuangalia nini kimesemwa badala ya nani kasema ili kufanyia kazi na kufikia malengo.

Amesema ushirikiano ni nyenzo muhimu itakayosaidia kuleta mafanikio katika Jimbo hilo, na kuongeza kuwa ”Mama Samia amesema acheni wapinzani waseme tunachokiona cha kweli kitekelezwe linaloonekana ni porojo litupieni mbali lakini wasitukane. Na hii imesaidia kwani zile kero tunazoziainisha kwa ushirikiano zimekuwa zikifanyiwa kazi kusema ukweli.”

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Mwaka 2024 Chama chake cha ACT – Wazalendo kimejipanga vyema kuhakikisha kinapata Viongozi wengi ili waweze kuwa na sauti ya kuwasemea Watanzania na kwamba kama chama hicho kitakuwa na mambo kama ya utawala wa CCM pia atakihama chama hicho lakini hatajiunga na kile kilichopo madarakani (akimaanisha CCM).

TANESCO wapewa agizo mapungufu Kituo cha Huduma
Dodoma Jiji yatangaza tahadhari Ligi Kuu Bara