Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amechukizwa na tabia ya baadhi ya watendaji sekta ya Ardhi wasiokuwa wema ambao wamekuwa wakiwahonga baadhi ya viongozi kwa kuwapa viwanja kama kinga mara wanapokutwa na makosa.

Silaa ameyasema hayo mara baada ya kufika eneo lenye mgogoro linalomilikiwa na Kanisa la Morovian kiwanja namba 1,2 na 3 Block T Mtaa wa Itega, jijini Dodoma.

Amesema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru anahusika kwa kiasi kikubwa na dhuluma za viwanja jijini Dodoma, kwani kuna makosa aliyoyatenda kwa kutumia cheo chake kama Mkurugenzi kudhulumu haki za wengine.

‘’Kuna wakati Wakurugenzi wa Mamlaka za upangaji na watendaji Wizarani ambao wamekuwa wakipima viwanja kwa watu wenye nguvu na kuacha kumpimia ardhi ambaye hana nguvu, katika uongozi wangu kama Waziri mwenye dhamana nitaweka mstari uliyonyooka na sitashiriki katika dhammbi kama hii.’’ Alisema Waziri Silaa.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Morovian amemshukuru Waziri Silaa na Serikali kwa ujumla kwa kufika eneo la tukio na kutatua mgogoro uliokuwa ukiwakabili, kwani wameteseka kwa kipindi kirefu bila kuwa na mafanikio.

Dodoma Jiji yatangaza tahadhari Ligi Kuu Bara
Mtibwa Sugar inavyojitafuta Ligi Kuu Bara