Waziri wa Nishati wa Niger, Mahaman Moustapha Barke amesema Taifa hilo limeanza kuendesha mtambo wake mkubwa wa umeme wa jua, baada ya nchi jirani ya Nigeria kuacha kupeleka vifaa vya umeme kufuatia vikwazo kutokana na mapinduzi ya Julai.

Barke ambaye alikuwa akionelea tukio hilo kupitia Televisheni ya Taifa amesema Kampuni ya Kitaifa ya umeme ya Nigelec tayari imeweza kuboresha ubora wa huduma, katika mji Mkuu Niamey na miji ya Dosso na Tillaberi.

Amesema, Nishati ya jua inapatikana kwa wingi katika nchi isiyo na bandari taifa la Afrika Magharibi ambalo sehemu kubwa ni jangwa na Kituo hicho kina vifaa vya umeme wa jua zaidi ya 55,000 na kina uwezo wa kuzalisha megawati 30 za umeme.

Aidha, Barke ameongeza kuwa kituo hicho pia kilitarajiwa kufanya kazi kuanzia Agosti 25 lakini kuanza kwa shughuli hiyo kulicheleweshwa baada ya wafanyakazi wengi wa kiufundi kuondoka kufuatia mapinduzi hayo.

Serikali yabainisha mikakati ustawi wa Walemavu
Ahmed Ally: Nyakati ngumu zinatukomaza