Uongozi wa Klabu ya Real Madrid upo tayari kuanza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na Carlo Ancelotti, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu 2023/24.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Relevo, Los Blancos inapanga kuanza mazungumzo kabla ya sikukuu ya mwaka mpya kwani mabosi wameridhishwa na mwenendo wao bora msimu huu.

Madrid inajiandaa kumpa mkataba wa miaka miwili Ancelotti mwenye umri wa miaka 64, licha ya kuhusishwa na timu ya taifa ya Brazil.

Brazil na Madrid ziko kwenye mvutano juu ya mustakabali wa Kocha huyo kutoka nchini Italia, huku Brazil ikidai Ancelotti amekubali kazi ya kuinoa timu hiyo ya taifa hilo kwa ajili ya michuano ya Copa America 2024, lakini Muitaliano huyo amekataa kuzungumzia suala hilo.

Wakati huo huo, Taarifa zimeripoti Madrid inamtizama kocha wa timu ya Argentina, Lionel Scaloni kama mrithi sahihi wa Ancelotti.

Scolari anatajwa kuwa mmoja wa makocha bora dunia baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Argentina na hivi karibuni aliwafunga Brazil bao 1-0 kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Hata hivyo, kocha huyo Muargentina alishindwa kuzungumza kuhusu hatma yake katika kikosi cha Argentina na kuhusishwa na Madrid.

Inajulikana Scolari mwenye umri wa miaka 45 ana urafiki wa ukaribu na nyota wa timu ya Argentina Lionel Messi, alianza kukinoa kikosi hicho baada ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

Scaloni aliichezea Argentina kwa mara ya kwanza mwaka 2003, na alikuwepo katika kikosi cha Argentina kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka yaliyofanyika mwaka 2006.

Al Ahly kutua Dar es salaam kesho Alhamis
Ajali ni Ugonjwa usioambukiza - RSA