Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Chama Cha kikomunisti cha China – CPC, kimekumbuka mchango wa Tanzania wa kuisaidia kurudishiwa kiti chake katika Umoja wa mataifa – UN Mwaka 1973 kufuatia Ujumbe kutoka nchini China ulipofika Ofisi ya CCM kibaha Mji, kukagua shughuli za uzalishaji wa bidhaa za CCM ikiwemo Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere.

Akihutubia Viongozi na wanaCCM wa ngazi ya Wilaya na mkoa wa Pwani walipofika katika Ofisi ya CCM Kibaha mjini, Komredi Mao Dingzhi, Naibu Waziri wa Idara ya Oganaizesheni ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China – CPC amesema, nchi za Afrika ikiwemo nchi ya Tanzania ambayo ilikuwa kinara wa harakati za kuhakikisha kiti cha China kinarejeshwa katika Umoja wa mataifa UN.

Amesema, mambo mengi ya maendeleo yanayoyafanya nchini na Taifa la China ni kukumbuka na kulipa fadhila za jitihada zilizofanywa na CCM na nchi ya Tanzania chini ya Uongozi imara wa Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuhakikisha kiti cha Taifa la China katika Umoja wa mataifa kinarejeshwa.

“CPC na Taifa la China wanakumbuka na kuthamini mchango huo wa Tanzania kupitia Balozi wake wakati huo katika Umoja wa Mataifa, Dkt. Salim Ahmed Salim, uliofanikisha kiti cha taifa la China kurejeshwa katika Umoja huo,” alisema Dingzhi.

Aidha, amesema uhusiano wa Tanzania na China kwa maana ya CPC na CCM ulianza miaka mingi iliyopita na kutaja mchango wa China kwa Tanzania kuwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia TAZARA na pia alitaja ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwaka jana katika nchi ya China hivyo Rais wa Taifa la China Xi Jinping anaona uhusiano wa Tanzania na China kuwa ni wamuhimu sana katika mataifa hayo.

Akizungumzia muundo wa Chama Cha kikomunisti nchini China CPC baada ya kusomewa taarifa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini Komredi Mao alisema muundo wa Chama hicho unaanzia ngazi ya chini kwenda ngazi ya juu kama kilivyo CCM ambapo pia CPC hutilia mkazo sana ngazi ya chini ya Uongozi kuwa na nguvu zaidi ya ngazi za juu za Chama kimaamuzi.

Akiwa katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere kwa mfipa Kibaha Pwani, Komredi Mao alitembelea na kukagua majengo ya Shule hiyo ambayo ujenzi wake upifadhiriwa na CPC na kubufaisha viongozi vijana wa nchi sita za kusini mwa Afrika ambazo zilishiriki harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika na kumshukuru kwa matunzo mazuri yanayoendelea katika kuhifadhi mazingira ya maeneo ya shule hiyo.

Aidha, alimkabidhi Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere Prof. Marceline Chijoriga vitabu Nane vya masuala ya Uongozi ambavyo vinaelezea namna ambavyo Taifa la China lilivyopiga hatua za maendeleo ili na viongozi wa nchi hizo sita zinazofika kusoma shuleni hapo waweze kujifunza ili nao wapige hatua za maendeleo.

Mkurugenzi, Watumishi wanusurika kifo ajalini
Simba SC yaishtukia Jwaneng Galaxy