Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida anatarajiwa kuwatimuwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali yake wapatao 15, sambamba na Viongozi wengine wa Ngazi za juu Serikalini, wanaochunguzwa kwa kukutwa na tuhuma za rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti maarufu Nchini humo la Asahi Shimbun, limeeleza miongoni mwa wanaokabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa ni pamoja na KatibuMkuu Kiongozi, Hirokazu Matsuno na Waziri wa Uchumi, Viwanda na Biashara, Yasutoshi Nishimura.

Aidha, Viongozi wote waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo ni kutoka kambi ya Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe, ambao wanatajwa kuwa ni wale wanaowania ushawishi ndani ya chama tawala cha LDP.

Katika sakata hilo, Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba kambi hiyo ilishindwa kutoa taarifa juu ya maelfu ya dolla ilizopata kupitia uchangishaji.

Young Africans yampeleka Ibrahim Mutaz CAF
Guardiola afichua siri ya ushindi Man City