Tabora United iko kwenye mazungumzo na kiungo mkabaji Mnigeria Emotan Cletus kutoka Sunshine Stars kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema tayari amewasili nchini na kuanza mazungumzo juu ya usajili, huku Kocha Mkuu Goran Kopunovic akiachiwa uamuzi wa mwisho kama ataridhishwa na kiwango chake.

“Ni kweli yupo nchini, lakini suala lake bado halijakamilika kwa sababu uamuzi wa mwisho haujafikiwa.

Ni mchezaji mzuri tunayeamini atatusaidia ila kama nilivyosema itategemea na makubalino yetu na yeye ya kimaslahi,” kilisema chanzo.

Mnigeria huyo ni wa pili kutua nchini kwa ajili ya mazungumzo na Tabora huku wa kwanza akiwa mshambuliaji Barine Eko aliyetokea Akwa United.

Azam FC kushusha vyuma viwili dirisha dogo
JKT Tanzania yavuta kifaa kutoka Zenji