JKT Tanzania inaendelea kuimarisha kikosi kwenye usa jili wa dirisha dogo na tayari imemalizana na straika wa IKU ya Zanzibar, Gamba ldd Matiko anayemiliki mabao sita katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Ingawa haijajulikana kasaini mkataba wa muda gani, Matiko atajiunga na JKT Tanzania muda wowote.

Mchezaji huyo ambaye ni kinara wa mabao JKU inayoongoza ZPL kwa ponti 36 ikiwa imefung mabao 21.

Gamba ldd alianza kufuatiliwa na JKT Tànzania baada ya kuifunga Singida Fountain Gate katika Kombe la Shirikisho Arika.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo alisema kupitia usajili unaoendelea wataongeza wachezaji wanne, lakini pia wapo ambao watakatwa kwa kutoonyesha ubora.

Ukiondoa Kichuya ambaye tayari kasaini, alisema kuna Matiko na wengine wawili ambao bado wanazungumza nao na mambo yakiwa tayari watajiunga na timu.

Mido Mnigeria aibukia Tabora United
Idadi ya waliofariki kwa mlipuko wa Lori yaongezeka