Mwenyekiti wa Mitume na Manabii Mkoa Manyara, Nabii Faraja Lucas akiongozana na manabii wengine kutoka katika maeneo mbalimbali, wamefika Kijijini Ngendabi kilichopo Katesh Wilayani Hanang’ kujionea madhara yaliyotokana na maporomoko ya tope, Mawe na Maji yaliyo tokea Desemba 3, 2023.

Akizungumza mara baada ya kufika Kijijini hapo, Nabii Faraja amesema wameguswa na tukio hilo hivyo wanatoa pole pamoja na kufanya maombi matakatifu katika eneo hilo.

Wakitoa shukrani kwa ujio huo na huduma ya maombi, mmoja wa wakazi wa eneo hilo Emmanuel mgendi amesema wanaishukuru Serikali pamoja na madhebu mbalimbali mbalimbli kwa kufika katika eneo hilo.

Mashirika ya Umma, Binafsi, Taasisi mbalimbali za Serikali na watu binafsi, wamekuwa wakifika Wilayani Hanang’ ili kutoa pole na kufikisha misaada kwa ajili ya waathiriwa huku wakiwapa pole kwa kuwapoteza ndugu na jamaa zao.

Kocha Benfica aionya Man Utd
Mbivu na mbichi kujulikana Simba SC