Timu ya soka ya taifa ya Nigeria imepata pigo katika harakati zake za kuwania taji la nne la Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’, baada ya kiungo wake mahiri kuondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano hiyo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 alikosa mchezo wa Championship wakati timu yake ya Leicester ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Huddersfield Town Jumatatu kwa majeraha ambayo hayakuwekwa wazi.
Msemaji wa timu ya taifa ya Nigeria, Babafemi Raji amesema kiungo Alhassan Yusuf, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora na timu ya Ligi Kuu ya Ubelgiji ya Royal Antwerp atachukua nafasi ya Ndidi.
Yusuf hajaiwakilisha Nigeria kwenye michuano yoyote lakini alikuwemo kwenye orodha ya awali ya wachezaji 40 kwa ajili ya michuano hiyo.
Mchezaji Kelechi Iheanacho anayekipiga kwenye klabu ya Leicester na Ndidi alisema anatarajia kuwa fiti kwa mashindano hayo baada ya kupata maumivu ya misuli.
Mabingwa hao mara tatu wa AFCON wameweka kambi yao Falme za Kiarabu kwa ajili ya mashindano hayo.
Nigeria wamepangwa Kundi A lenye timu za Ivory Coast, Guinea Bissau na Guinea ya Ikweta. Watacheza mchezo wao kwanza dhidi va Guinea ya Ikweta Januari 14.