Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema sheria mpya ya uwekezaji ya mwaka 2023 itakuwa bora Afrika ambayo ataisaini hivi karibuni baada ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi Mwezi Novemba Mwaka jana.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo hii leo Januari 7, 2024 mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Hoteli ya nyota tano ya Zanzibar Crown Mazizini, Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi ñ.

Amesema, anawapongeza wawekezaji wa hoteli hiyo kwa kuwekeza dola za kimarekani Milioni 30 kwa mradi wa hoteli ambapo utatoa fursa ya ajira ya Wazanzibari zaidi ya 200.

Rais Dkt. Mwinyi pia ameeleza kuwa lengo la Serikali ni kwamba ifikapo mwaka 2025 ipokee watalii milioni moja ambapo sasa Zanzibar inapokea watalii laki tano na elfu sitini kwa mwaka.

Ameongeza kuwa, Zanzibar inaongoza kupokea ndege nyingi Tanzania kwa sasa ukilinganisha na viwanja vya ndege vya Kilimanjaro na Dar es Salaam.

NECTA yatangaza Matokeo Kidato cha Pili, la Nne
NHIF yakanusha taarifa za uzushi mtandaoni