Baraza la Mitihani Tanzania – NECTA, limetangaza matokeo ya kitaifa ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika mwaka 2023 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.13 kwa kidato cha pili na asilimia 0.39 kwa darasa la nne.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Said Mohamed amesema wanafunzi 1,287,934 sawa na asilimia 83.34 wamefaulu kuendelea na darasa la tano kutoka darasa la nne.

Upande wa kidato cha pili, wanafunzi 592,741 ambao ni sawa na asilimia 85.31 wamefaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne na kwamba Baraza hilo limefuta matokeo ya Wanafunzi wa Watatu wa darasa la nne na 14 wa kidato cha pili ambao waliandika matusi.

Ili kutazama matokeo yote waweza fungua link ifuatayo;

https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/ftna/ftna.htm

Polisi wafanikisha Mtoto Eric kuingia Darasani
Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar kuwa bora Arfika