Novemba 23, 2023 iliripotiwa taarifa inayomhusu Erick Hongera (6), Mkazi wa kata ya Bilo Wilayani Malinyi ambaye alikuwa na kawaida ya kukaa kando ya majengo ya shule ya Msingi Mnga Juu akiwa mpweke baada ya wazazi wake kushidwa kumudu mahitaji ya kumpeleka shule mtoto huyo.

Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi kupitia Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha, limefanikiwa kuwasilisha msaada wa mahitaji ya shule ikiwemo sare za shule, viatu na begi, ili kumwezesha kuanza shule 2024.

Mama Mzazi wa Mtoto Erick, Consolata Jerimanusi amelishukuru Jeshi hilo kwa kufanikisha Mwanae kuanza shule na kutoa wito wenye watoto wenye uhitaji kama huo kutoa taarifa ili waweze kusaidiwa.

Ni wazi kuwa jambo hili ni mfano wa kuigwa na Jeshi la Polisi kupitia kwa wahusika waliofanikisha jambo hilo wanapaswa kupewa kongole kwa kuthamini hitaji muhimu la mtoto huyo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 8, 2024
NECTA yatangaza Matokeo Kidato cha Pili, la Nne