Wizara ya elimu nchini Zambia imesema wanafunzi wote watachelewa kurejea shuleni kwa wiki tatu kutoka likizo kutokana na mlipuko wa kipindupindu.

Hayo yamejiri baada ya Wizara ya afya nchini humo kutangaza visa 3,015 vya kipindupindu na vifo 98 vimerekodiwa tangu Oktoba 2023, kutokana na ugonjwa huo.

Aidha, Wizara ya elimu imesema wanafunzi wote nchini Zambia wa shule za msingi na sekondari walitarajiwa kurejea jumatatu lakini sasa watarejea tena Januari 29

Hapo awali Wizara ya Afya ilikuwa imeonya kwamba mlipuko huo unatishia usalama wa afya wa nchi.

 

 

Kikosi kazi Taifa Stars AFCON 2023
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 8, 2024