Afarah Suleiman – Manyara.
Ikiwa Leo ni siku ya pili tangu kufunguliwa kwa Shule zote Nchini, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewataka Wazazi na Walezi Mkoani humo, kuhakikisha wanawapeleka Wanafunzi wote walio andikishwa shule kabla ya January 11, 2024.
Sendiga ameyasema hayo katika mkutano na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa ya Wanafunzi kuripoti Shuleni katika Mkoa wa Manyara kwa Shule za Msingi na Sekondari na kudai kuwa kwa Elimu ya awali walioripoti ni Wanafunzi 27,239 wakiwemo Wavulana 13,893 na Wasichana 13,346 ambao ni sawa na asilimia 73 ya waliosajiliwa mwaka 2024.
Kwa upande wa Shule za Msingi walioripoti ni 35,298 wakiwemo wavulana 17,886 na Wasichana 17,412 sawa na asilimia 72 ya waliosajiliwa ambao ni wafunzi 49,038.
Kwa Shule za Sekondari, walioripoti ni Wanafunzi 2,917 wakiwemo Wavulana 1,293 Wasichana 1,624 ambapo waliopagwa kuanza katika Shule za kata kwa mwaka 2024 ambao ni Wanafunzi 31,344.
Aidha, Sendiga amesema Mkoa umejipanga kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Elimu Bure, na kuweka mikakati mbalimbali, Ili Wanafunzi wote waliopangiwa kuripoti shule waweze waanze masomo.