Akina mama wa Kijiji cha Minazi Mikinda, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, Mkoa wa Pwani wamehimizwa kuwa walinzi wa watoto wao walio katika umri wa balehe.

Wito huo, umetolewa na Polisi kata wa Ruvu stesheni, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Sheila Msami, katika kijijini hicho wakati akitoa elimu ya muongo rika, kwa vijana na akina mama.

Amesema, akina mama wanatakiwa wawe mstari wa mbele kuhakikisha Vijana wanakua na maadili mema kwa kuzungumza nao mara kwa mara na kuwakumbusha masuala mbalimbali, ikiwemo madhara ya kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo.

Aidha, Sheila pia aliwataka akina mama kujilinda wao wenyewe dhidi ya vitendo vya kikatili, ambavyo huanzia katika ngazi ya familia na kwamba wasisite kuripoti matukio ya kikatili katika kituo cha Polisi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kwa haraka.

Matukio ya uhalifu: Bajaji zanyooshewa kidole
Zaidi ya 6,000 wafariki wakijaribu kwenda Ulaya