Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema suala la  mchakato wa katiba kwenye nchi yeyote sio wa mwaka mmoja.

Kinana ameyasema hayo hii leo Februari 4, 2024 katika Mkutano wa Wanachama na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuongeza kuwa mchakato huo una mageuzi madogo kwenye katiba na sheria zimepelekwa Bungeni.

Amesema, “sheria ya Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais, sheria ya Tume ya Uchaguzi na mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa, lengo lake ni kuboresha uchaguzi wa mwaka 2024 na 2025.”

Aidha, Kinana ameongeza kuwa, “Uchaguzi sio tume tu, uchaguzi ni sera, kujipanga, kujieleza, kusikiliza watu pamoja na kuwa na muundo mzuri wa uchaguzi ndani ya Chama chako.”

Polisi ataka Wananchi wamuogope Mungu
Tunashughulikia changamoto za Walimu - Mchengerwa