Wabunge nchini Senegal wamepiga kura ya kuunga mkono muswada wa kuahirisha uchaguzi mkuu, ambao umepangwa kufanyika Desemba 15, 2024, hatua ambayo itamuwezesha Rais Macky Sall ambaye anakamilisha mihula yake miwili ya kusalia madarakani.
Hatua hiyo, ilitanguliwa na baadhi ya Wabunge wa upinzani kuzusha vurugu ili kujaribu kukwamisha mchakato huo, lakini idadi ya Wabunge 105 kati ya 165 walifanikisha lengo la muswada huo.
Hata hivyo, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Taifa hilo kuahirisha uchaguzi, jambo ambalo limezusha hasira na vurugu kutoka upinzani wanaodai kuwa maamuzi hayo ni sawa na mapinduzi.
Maandamano mapya mjini Dakar yalifanyiak na kupelekea hadi baadhi ya shule kufungwa kutokana na kile wanachodai kupinga hatua hiyo, ambapo awali, uchaguzi wa Rais ulikuwa umepangwa kufanyika Februari 25, 2024.