Inaelezwa kuwa Real Madrid wanaendelea kufanyia kazi mkataba wa Kylian Mbappe kwa kujiamini kwa asilimia zote, lakini bado hajasaini.

Real Madrid wanaamini Mbappe anataka wahakikishe wanamaliza suala hili mwaka huu, lakini bado ni mapema kusema dili limekamilika au amesaini.

Uamuzi rasmi wa upande wa wachezaji unatarajiwa kuweka wazi hivi karibuni na pande zote zitamuona Mbappe akielezea mustakabali wake PSG.

Kuna makubaliano ya kiungwana kati ya Kylian na Rais wa PSG, Nasser Al Khelaifi tangu Agosti kwani Mbappé aligoma kupokea bonasi ya uaminifu ya euro milioni 80 endapo ataondoka.

Mbappe aliahidi kumjulisha mwenyekiti wa PSG Nasser Al Khelaifi punde tu atakapoamua mustakabali wake kuhusu mkataba unaoisha Juni 30, 2024.

Ikiwa Mbappé ataamua kusaini Real, mshahara utapungua sana kuliko ule ambao aliwekewa mezani mwaka 2022.

Mahundi: Mradi wa Maji Tukuyu kuhudumia wakazi 63,647
Dkt. Mwinyi atoa maagizo uanzaji kazi Mahakama ya Rushwa