Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameagiza taasisi zinazo husika na sheria kukamilisha mchakato wa utungaji wa sheria ili kuanza kazi kwa Mahkama Maalum ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi kwa mwaka huu.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar katika viwanja vya Mahkama kuu Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja hii leo Februari 7, 2024 na kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama (2024-2029) na kukabidhiwa ripoti ya utendaji kazi wa Mahakama ya mwaka 2023.
Amesema, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha mhimili wa Mahkama na Taasisi zote za Sheria ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi, hatua hizo ikiwemo ujenzi wa majengo saba ya Mahakama katika Mikoa na Wilaya Zanzibar, kuongeza idadi ya Majaji, Mahakimu na Makadhi pamoja na kuboresha maslahi kwa Majaji, Mahakimu, Makadhi na watumishi wengine wa Taasisi za sheria ili kuongeza ufanisi.
Rais Dk.Mwinyi ameongeza kuwa, ustawi bora wa wananchi utategemea kuwepo kwa misingi imara ya kuheshimu haki za binadamu, utawala bora, uhuru wa Mahkama pamoja na sheria madhubuti zinazoilinda jamii dhidi ya aina zote za unyanyasaji, huku akiipongeza Mahakama ya Zanzibar kwa kuanza mchakato wa kuboresha mfumo wa kieletroniki wa usikilizaji wa mashauri kwa msaada wa kitalaamu kutoka Mahakama ya Tanzania.

Real Madrid yachizika kwa Mbappe
Deco: Hatujampata mrithi wa Xavi