Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Sarafiphine Mwanakulya mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi anaomba msaada wa matibabu kwa ajili ya mtoto wake mwenye umri wa miezi 10 anayesumbuliwa na maradhi ya moyo pamoja na hernia (Ngiri).
Maombi hayo aliyawasilisha katika mkutano wa mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Inyonga mjini, ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Alhaj Majid Mwanga, ambapo Sarafina anasema mtoto wake anasumbuliwa na uwepo wa matundu mawili kwenye moyo huku matibabu yake yakihitaji zaidi ya shilingi milioni1 13.
Mkuu wa wilaya hiyo, Majid Mwanga alimkabidhi kiasi cha sh 210,000 kwa ajili ya matumizi na dawa za kutumia.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameahidi kukuatana na Bi. Sarafina kuona namna gani ya kulitatua tatizo lake ili kumuokoa Mtoto anayeumwa ambapo mama huyo ameomba msaada kwa wasamaria wema kwa yeyote atakayeguswa anaweza kuwasiliana nae kwa namba +255 744 693 443 jina Saraphine Paul Mwanakulya