Kiungo Mkabaji kutoka DR Congo na Klabu ya Simba, Fabrice Ngoma amewapa masharti uongozi wa klabu hiyo, kama wanataka aendelee kusalia kikosini hapo, wasajili wachezaji wenye moyo wa kuipambania timu.
Hivi karibuni kulikuwepo na tetesi za staa huyo kuletewa ofa na Pyramid, Al Alhy na Raja Casablanca, ila alitaka maombi hayo yapelekwe kwa uongozi wa Simba SC, kutokana na kuwa na mkataba wa mwaka mmnoja klabu ya Simba SC.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi zinasema kuwa, viongozi walikaa na staa huyo mezani na kujua anahitaji kitu gani ili aweze kubaki, ndipo alipotaja vitu viwili muhimu.
“Alisema anataka kuona Simba SC inachukua mataji. Hivyo tutasajili wachezaji wenye moyo wa kujituma na uchungu na timu.” alidokeza kiongozi huyo na kuongeza;
“Amesisitiza anaona ndani ya kikosi hicho ameona wachezaji wachache wa kigeni ndio wenye moyo wa kuipambania timu jambo linalomuumiza kuona wakati anarejea mapumziko nchini kwao anakuwa hana furaha.” aliongeza.
Amesema hakuna mchezaji anapenda kucheza timu ambayo haina mafanikio kama kutwaa mataji na kufikia malengo ya mwanzo wa msimu kama wanavyokubaliana.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa kiungo huyo alitua Simba SC kutokana na mafanikio makubwa waliyoyapata ndani ya misimu minne mfululizo ambayo timu hiyo ilitwaa mataji mfululizo na kuwa na mafanikio kimataifa.
“Mchezaji anapenda mafanikio anapenda timu ipate mataji ishiriki michuano ya kimataifa na aliamini kuwa akiwa ndani ya Simba atapata mwanya wa kutoka hapo na kwenda kujaribu maisha mengine kutoka nje.” kimesema chanzo hicho