Imefahamika kuwa Kocha wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City Pep Guardiola huenda akaondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu ujao.

Guardiola anatarajiwa kuondoka klabuni hapo, kufuatia kugoma kusaini mkataba mpya, baada ya kufanikisha safari ya mafanikio ya kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya nne mfululizo.

Taarifa zilizoripotiwa na Gazeti la The Mail zinaeleza kuwa, Uongozi wa Manchester City ulikuwa kwenye mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya Kocha huyo kutoka nchini Hispania, lakini mpango huo umefifia.

Kutokana na dalili hizo, Uongozi wa Manchester City utalazinmika kumsaka Kocha Mkuu mpya mwishoni mwa msimu huu, endapo mazungumzo baina ya pande hizo mbili hayatazaa matunda.

Hadi sasa Guardiola ameiwezesha Manchester City kutwaa mataji sita kati ya saba ya Ligi Kuu ya England, huku wakishinda Mataji Matatu ‘Treble’ msimu uliopita 2022/2023.

Mayele afunguka kurudi Young Africans
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 27, 2024