Gwiji wa Soka nchini Ufaransa Fabian Barthez amesema shujaa mwenzake Thierry Henry amepanga kutwaa Medali ya Dhahabu kwenye Michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini Paris 2024, kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11.

Henry ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa wakati kikitwaa Ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1998, ana jukumu la kuhakikisha timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo inapambana na kutwaa Medali ya Michuano ya Olimpiki.

Barthez ambaye alikuwa sehemu ya mafanikio ya mwaka 1998 amesema anaamini Henry ana nafasui kubwa ya kufanya maajabu kwenye Michuano hiyo, huku akitarajia ushirikiano kutoka kwa watu mbalimbali wa Ufaransa.

“Bila shaka watu wanamtarajia Henry kutwaa Medali ya Dhahabu ya Olimpiki. Binafsi ninaamini anakwenda kufanya jambo kubwa sana katika Michuano hiyo, kwa hivyo sina wasiwasi naye. Nina ukaribu mkubwa na Henry, na ninamtakia kila la kheri na ninatumai kwamba atafanikiwa.”

EXCLUSIF. Fabien Barthez : "Pourquoi je soutiens Michel Moulin pour  l'élection à la FFF"

Gwiji wa Soka nchini Ufaransa Fabian Barthez

“Ni Michuano ya Olimpiki, kwa hivyo ni tukio la kimataifa. Tunapaswa kujivunia cha kwetu kwanza, kwa kuamini kinakwenda kufanya maajabu makubwa, ndio maana nimemtanguliza rafiki yangu Henry kwa kuamini anaweza.

“Pia ninawatakia kila la kheri wanamichezo wote watakaoiwakilisha Ufaransa katika Michuano hii, kwa hakika ninaamini wamejiandaa vizuri kwa lengo la kuiletea sifa nchi yetu ambayo ndio mwenyeji.” amesema Barthez

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 25, 2024
Xavi Hernandez atimuliwa FC Barcelona