Uongozi wa FC Barcelona umetangaza kusitisha mkataba wa Kocha Mkuu Xavi Hernandez leo Ijumaa (Mei 24), baada ya mazungumzo ya pande hizo mbili kwenda vizuri na kufikia tamati kwa makubaliano maalum.

Xavi ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, huku uamuzi mkubwa wa Uongozi wa Barca kusitisha mkataba wake umetokana na klabu hiyo kushindwa kufikia malengo yake msimu huu 2023/24.

“Rais wa FC Barcelona Joan Laporta amemwambia Xavi Hernandez hataendelea kuwa kocha kwa msimu wa 2024-25,” imesema taarifa ya Barcelona

Lengo Kuu klabuni hapo lilikuwa kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ lakini mambo yaliwaendelea hovyo na taji hilo kubebwa na wababe wa mjini Madrid (Real Madrid).

FC Barcelona pia imeshindwa kufikia lengo la kutwaa Ubingwa wa Kombe la Mfalme ambalo limekwenda kwa Athletic Bilbao, huku ikitolewa katika hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa kufungwa na PSG ya Ufaransa.

Awali Xavi alitangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, lakini baadae alibadilisha msimamo wake na kutaka kuendelea kufanya kazi kama Kocha Mkuu kwa mujibu wa mkataba wake.

Maamuzi hayo aliyafanya siku kadhaa zilziozpita lakini imekuwa bahati mbaya hajabahatika kuyatumikia kwa vitendo, kutokana na uongozi wa juu kumgeuka na kumtaka kuondoka klabuni hapo.

Thierry Henry atabiriwa makubwa Olimpiki 2024
Rais Hussein Mwinyi aishukuru CAF