Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)  kwa kuifanya Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya African Football Championship  mwaka huu.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Rais wa Shirikisho la  Soka barani Afrika (CAF), Dk.Patrice Motsepe  na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar  itaendeleza na kudumisha uhusiano wake  na CAF .

Rais Dk.Mwinyi amemueleza Dk.Motsepe  kuwa Zanzibar inahitaji msaada wa kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi za academy kwa kushirikiana na  CAF.

Rais wa CAF Dk.Motsepe leo  atashuhudia mchezo wa kwanza wa fainali za Mashindano ya African  Schools Football Championship yanayofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Xavi Hernandez atimuliwa FC Barcelona
DC Buswelu: Maendeleo yatawapa morali walipa kodi