Johansen Buberwa – Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kuwa watulivu na kuzingatia taratibu uchaguzi ikiwemo kusubiri matokeo.

Akizungumza baada ya kumalikiza kupiga kura kwenye kituo cha uwanja wa ndege katika mtaa wa pwani kata miembeni hii leo Novemba 27, 2024 Hajjat Mwasa amesema asiwepo mtu yoyote anaye jaribu kuleta vurugu maana haiendani na utamaduni, mila na desturi za mkoa huo.

“Mkoa wa kagera unasifika kwa ustarabu,utulivu,busara na hekima hatuwezi kukubali wala kuruhusu zoezi la uchaguzi litugombanishe kila kitu kitakuwa salama,” amesema Hajjat Mwassa.

Mkoa wa Kagera una zaidi ya wapiga kura milioni 1.5 na vituo vya wapiga kura 4012.

Rais Samia: Watanzania washiriki uchaguzi kwa adabu, faragha
Uchaguzi Serikali za Mitaa: Babati waitika, utulivu watawala