Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania washiriki uchaguzi kwa adabu na faragha ili uvunjifu wa amani usiwepo.

Dkt. Samia ameyasema hayo leo Novemba 27, 2024 wakati akishiriki upigaji kura kwenye kituo cha sokoine Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.

Amesema, “niwakumbushe tu twendeni tukapige kura kwa faragha,utulivu na adabu,tusivunje amani yetu tuliyonayo,mkapige kura kwa maelewano, na masanduku yanavyosema ndio hivyo hivyo.”

“Matumaini yangu ni mtapiga kura salama na kwa mtamalliza salama, na mpaka sasahivi naona mambo yanakwenda vizuri, na leo watanzania watafanya chaguzi zao za kuchagua watu wao wenye uwezo wa kuwafanyia kazi zao,” amesema Dkt. Samia.

Hata hivyo, Rais Samia amesema kura ni mtindo wa Demokrasia na utamaduni wa Siasa ambapo amewataka watanzania kupiga kwa maelewano kuchagua viongozi wenye sifa.

“Jana nilitoa maelezo marefu kwa Waganzania kuwa wote wenye sifa watoke wakapige kura na nadhani wameitikia wito, kwasababu hapa nimeona watu wengi kidogo wamejitokeza kupiga kura,” aliongeza Rais.

DC. Lulandala awapa neno Wananchi Uchaguzi Serikali za Mitaa
RC Mwasa ataka utulivu, uzingatiaji taratibu za Uchaguzi