Ingawa maua ni sehemu ya mapambo makuu ya msimu huu wa Christmas ndani na nje ya nyumba zetu, tunapaswa kuchukua tahadhari kwani baadhi ya maua hayo yanaweza kutudhuru yasipochukuliwa kwa umakini unaotakiwa.

Dar24 imezungumza na mtaalam wa maua ambaye pia anafanya biashara hiyo katika eneo la Mbuyuni jijini Dar es Salaam, Mzee Rashid Bakari, ambaye ametaja baadhi ya maua ambayo yanaweza kugeuka sumu kwa mtumiaji.

“Sio kusema kwamba ni sumu ya vipi…. Ni yale yenye utomvu. Kama discuss flower, iters rose na mengine, hayo ni ya sumu, lakini yapo maua mengine ambayo sio sumu,” Mzee Rashid ameiambia Dar24.

“Yale…sumu yake ni kwamba unapaswa kuangalia isikudondokee kwenye macho. Ikikudondokea kwenye macho ina maana hali yako itakuwa sio nzuri,” aliongeza.

Dar24 inakukumbusha kuchukua tahadhali kwa hasa kwa watoto wako kuhusu maua yanayozunguka nyumba yako, japo yanavutia yanaweza kuwa tatizo endapo watoto watachezea utomvu wake.

Angalia video hii kwa maelezo zaidi:

Lowassa afunguka maisha nje ya CCM, ‘Sikutegemea ingekuwa hivi’
Anayetajwa kumvaa Pacquiao ajitangaza kuwa ‘bondia wa mwaka 2016’