Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amewataka vijana kushiriki katika mikutano mbalimbali ya vijiji ili waweze kutambua fursa za kimaendeleo, ikiwemo ujasiliamali, badala ya kukaa vijiweni na kuendekeza migomo na kushawishiana kuacha kuhudhuria mikutano hiyo.

Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kutembelea vijiji mbalimbali kwaajili ya kufanya mikutano iliyolenga kutoa taarifa ya mapato na matumizi, ambapo wafanyabiashara na vijana waligoma kuhudhuria.

Aidha, Ridhiwani amesema  kitendo cha vijana na baadhi ya wakazi hao kutohudhuria mikutano kwenye eneo lao, kunasimamisha maendeleo.

“Nilipofika ofisi ya kijiji hiki, mkutano haukufanyika kwa madai ya wananchi kuugomea, wakidai kwanza lizungumziwe suala linalohusu mgogoro wa ardhi kati yao na mmoja wa mkazi anayeishi Dar es salaam, wakidai ni la muda mrefu  na halijapatiwa ufumbuzi,”amesema Ridhiwani.

Hata hivyo, Ridhiwani amewataka vijana kujitambua na kuacha kutumiwa kama ngazi ya baadhi ya watu kwaajili ya maslahi yao binafsi.

Majaliwa aonya ujenzi holela Kigamboni
Tanesco hali bado tete