Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha unasimamia ujenzi wa kisasa na kutenga maeneo maalumu ya wazi  katika Manispaa hiyo, ili kuepusha makosa ya ujenzi holela.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo jijini Dar es salaam, amesema kuwa tayari mkoa wa Dar es salaam umejaa na eneo la kigamboni ndio pekee la kukimbilia.

“Tunataka turekebisha makosa tuliyoyafanya katika mipango miji jijini Dar es salaam, zingatieni matumizi bora ya ardhi, jengeni Manispaa ya kigamboni iwe mji wa kisasa,”amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amesema Dar es salaam imejengwa bila kuzingatia mipango miji kiasi cha kukosa maeneo nyeti kama bustani ya kupumzikia wananchi pamoja na fukwe.

Wakurungenzi wengine Tanesco watumbuliwa
Ridhiwani: Vijana hudhurieni mikutano ya vijiji