Mwezi Oktoba, 1955 Serikali ya Kikoloni ilipitisha Sheria iliyowapunguzia kwa kiasi kikubwa uhuru wa kusema raia hasa Mwafrika.
Chama cha TANU ndiyo kilipambana kwa kuipinga vikali Sheria hiyo ya kibeberu, ambapo kilipeleka barua kwa Waziri Mkuu wa Makoloni Uingereza na katika Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, pia kilituma barua kwa Gavana ili kuueleza ubaya wa Sheria hiyo na kuomba isitumike kwani inakandamiza uhuru wa raia.
Katika picha hapo juu ni Baraza la Wazee wa TANU, Sheikh Suleiman Takadir wa pili chini kulia, wa pili waliosimama Dossa Azizi, wa sita Julius Nyerere, wa saba John Rupia, wa tisa Said Chamwenyewe anayefuatia Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate.