Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga aliyetambulika zaidi kwa jina la Mkwawa na aliyekuwa Chifu na kiongozi mkuu wa kabila la Wahehe mwishoni mwa karne ya 19 alipata umaarufu zaidi kwa kuongoza vita vya Wahehe dhidi ya Wajerumani, wakati huo Wajerumani wakiunda koloni lao Afrika Mashariki (Tanganyika, Rwanda pamoja na Burundi).

Jina la chifu Mkwawa ni kifupisho cha Mukwava ambalo tena ni kifupisho cha Mukwavinyika, lililokuwa jina lake la heshima likimaanisha “kiongozi aliyetwaa nchi nyingi”.

Chifu Mkwawa alizaliwa mwaka 1855 huko Luhota karibu na Iringa mjini. Alikuwa mtoto wa chifu Munyigumba aliyeaga dunia mwaka 1879, baada ya kifo cha chifu Munyigumba, watoto wake walishindania urithi wake na Mkwawa alishinda akawa kiongozi mpya.

Mkwawa aliondoka sehemu za Iringa kuelekea mto Ruaha mwezi Agosti 1896 alipoona mgawanyiko huku akilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na kumlinda dhidi ya vikosi vya Wajerumani waliomtafuta.

Mwaka 1898 Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu akiongozana na watu wachache sana. Aliishi hasa kwa njia ya kuwinda,

Mkwawa alibakia na walinzi 2 tu walioitwa Musigombo na Lifumika. Asubuhi ya Tarehe 19 Julai, Lifumika aliamua kukimbia. Lakini siku ileile alikutana na kikosi cha Wajerumani akakimbia lakini wakamshika wakamlazimisha kuwaambia habari za Mkwawa.

Kijana aliwaeleza Wajerumani mahali alipokuwa Mkwawa kuwa ni umbali wa masaa 3. Walimlazimisha kuwaongoza. Njiani walisikia kwa mbali mlio wa  risasi 1. Wakaendelea na baada ya masaa mawili walikuta maiti za Mkwawa na yule kijana mwingine. Inaonekana waliwahi kujiua na sauti ya risasi ilikuwa Mkwawa aliyejipigia risasi.

 

Somalia yapiga marufuku ndoa za kifahari, ni baada ya kugundua jambo
AU yatangaza kuchukua hatua kali dhidi ya Yahya Jammeh