Katika harakati za kupambana na kukomesha biashara ya madawa  ya kulevya katika Jiji la Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, ameendelea kutaja orodha ya majina ya watu wanao tuhumiwa kujihusisha na uuzaji madawa hayo na kuwataka kuripoti kituo cha Polisi cha Kati siku ya jumatatu kwa ajili ya mahojiano.

Makonda ametaja orodha ya majina hayo ya watuhumiwa wa uuzaji wa madawa ya kulevya huku akisema mkono wa serikali ni mrefu hivyo yeyote atakaebainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake.

Majina yaliyotajwa na wanaotakiwa kuhojiwa siku ya Jumatatu ni msanii wa bongo fleva Vanessa Mdee, Tunda, Omary Sanga ambaye ameelezwa kuwa amesababisha watanzania wengi kufungwa nchini China, Kashozi, Amani, Halidari Kavila pamoja na Askari Polisi 3.

Video: Taarifa ya jeshi la polisi kuhusu watuhumiwa wa uhalifu Dar
Makamba afungua mkutano wa tathmini ya athari za mazingira