Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata silaha aina ya Shortgun Majohe relini iliyokuwa ikitumiwa na majambazi katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Simon Sirro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, amesema kuwa silaha hiyo ilikamatwa baada ya majibizano ya risasi ya ana kwa ana kati ya askari polisi  na majambazi.

Katika majibizano hayo mtu mmoja alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi sehemu ya paja na kumsababishia maumivu makali amabayo yalipelekea kupoteza maisha.

Aidha, Sirro amesema kuwa Jeshi hilo la Kanda Maalum pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa sugu 186 wa makosa mbalimbali katika maeneo ya Mbagala,Buguruni,Kiluvya, Gongo la Mboto,Tandika,Ukonga,Banana,Kunduchi,Kawe na Keko.

Pia Sirro amewatahadharisha wananchi wa Jiji la Dar es salaam kuwa makini na mvua zinazotarajiwa kuanza kunyesha kwani zinaweza kusababisha madhara makubwa.

Hata hivyo ameongeza kuwa kikosi cha usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam cha ukamataji wa makosa ya usalama kwa kipindi cha kuanzia tarehe 27/o1/2017 hadi tarehe 01/01/2017 wamekusanya kiasi cha fedha shil.566,370,000/=

 

Video: Makonda alivyotaja majina ya Vanessa, Tunda, Polisi 3 tuhuma za madawa ya kulevya

Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala yawashukia wakuu wa mikoa na wilaya
Video: Vanessa,Tunda, Polisi 3 watajwa madawa ya kulevya