Wanyakyusa ni kabila la watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) kaskazini kwa Ziwa Nyasa.
Asili ya jina hilo la Wanyakyusa ni kutokana na jina la mke wa mtawala wa kimila au (chifu) aliyeitwa Kyusa, pia awali waliitwa Wasokile hiyo ni kutokana na salamu yao asali aliyosema sooki sooki nna!
Pia, #HapoKale Wanyakyusa walijulikana kwa jina la Wangonde au Wasochile. Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini kwa Ziwa Nyasa mwishoni mwa karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote “Wakonde” kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.
Hadi leo kanisa la Kilutheri la KKKT linatumia jina “dayosisi ya Konde” kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wangonde wengi walikuwa kaskazini mwa ziwa Nyasa, lakini katika harakati za maisha na mabadiliko ya mazingira wengi wao wakakimbilia Mbeya mjini na sehemu nyingine.
Mara nyingi Wangonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Mwaka 1993 watu zaidi ya milioni walikuwa wanajumlishwa kwa jina hili, takriban 750,000 upande wa Tanzania na 300,000 upande wa Malawi.
Wanyakyusa wapo wa aina mbili ambayo ni Wanyakyusa wa Tukuyu na Wanyakyusa wa Kyela. Wanatumia lugha ya Kinyakyusa (Kingonde)
Kinyakyusa (Kingonde) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wanyakyusa wanaokaa hasa Rungwe.
Kufuatia uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie, Kinyakyusa iko katika kundi la M30.