First Lady wa Young Money, Nicki Minaj amefanya tendo jema katika kijiji kimoja nchini India kwa kuwasaidia wanawake kupata huduma ya maji safi na vituo vya kujiendeleza kitaaluma na kiteknolojia.
Nicki ameweka picha wana kijiji hao katika mtandao wa Instagram huku akimshukuru kiongozi wa dini wa kijiji hicho kwa kusaidia kufanikisha ujenzi wa visima viwili vya maji safi, upatikanaji wa kituo cha kusomea kompyuta, kituo cha kujifunzia ufundi wa cherehani na jengo la kufanyia ibada.
VIDEO: Mwigulu ateta na Polisi mauaji Kibiti, JPM atoboa siri bomba la mafuta
“Ninajivunia dada zangu wa India. Mungu ni mwema. Hitaji lao lilikuwa kuwa na visima vya maji na sehemu ya kufanyia ibada, sehemu ambayo wangeweza kujifunza teknlojia, kompyuta, kusoma n.k. Hivi tumeanza tu. Hawa wanawake ni sisi na sisi ni wao!” Aliandika.
Aidha, rapa huyo ambaye alipost pia karatasi inayoonesha miamala ya fedha zilizotumwa kwa ajili ya kazi hiyo, alisema kuwa anaanzisha pia programu maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wasichana kujiendeleza kielimu.
Mwezi uoliopita, kupitia mtandao wa Twitter, Nicki Minaj pia alisaidia kulipa madeni na karo za baadhi ya wanafunzi waliokuwa kwenye mtandao huo na kuahidi kuwa litakuwa jambo endelevu.