Katika kuhakikisha kuwa wakulima wa tumbaku wanafaidika nchini, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji tumbaku kutoka Wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji unaotarajiwa kufanya na baadhi ya wakulima wasio waaminifu.
Aidha, Mwanri ametoa agizo hilo mjini Tabora wakati wa kikao cha wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na mambo mengine kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania kimejadili tarehe ya kuanza kwa masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii (26.5.2017) katika meneo mbalimbali.
Amesema kuwa Serikali iliamua wakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi katika maeneo yao na sio vinginevyo ili kuepuka watu wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni tumbaku ya wakulima wadogo wadogo walipo katika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao na kusababisha madeni katika vyama vyao vya Msingi.
Hata hivyo, ameongeza kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wa kutorosha tumbaku hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.