Leo Juni 12, 2017 Kamati ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa madini (Makanikia) iliyoundwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imewasilisha ripoti ya uchunguzi huo Ikulu Jinini Dar es salaam.
Katika ripoti hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Nehemia Osoro imebaini kuwa Kampuni ya ACACIA MINE PLC haikusajiliwa nchini wala haina hati ya usajili na inafanya biashara ya madini nchini kinyume cha sheria.
 Pia Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Nehemia amesema kuwa Serikali imepoteza Kodi ya Mapato ya kiasi cha sh. trilioni 55 tangu mwaka 1998 hadi Machi 2017 katika usafirishaji wa makinikia, bilioni 94 Kodi ya Zuio ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 na kufanya Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 kwa Kiwango cha wastani ni trilioni 188.58.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 13, 2017
Video: Rais Magufuli aagiza mikataba ya madini kupitiwa upya, ahoji aliyetuloga