Polisi nchini Nigeria wameagiza kumkamata msanii mkongwe wa muziki nchini humo, Peter Okoye wa P-Square kwa tuhuma za kuwatukana viongozi wa serikali kuwa ni wendawazimu na wajinga.

Peter aliporomosha maneno hayo yasiyo na nidhamu kwa viongozi wake kutokana na tamko la marufuku lililotolewa na viongozi hao kuhusu wasanii wote wa muziki na filamu nchini Nigeria kutoshuti kazi zao nje ya Nigeria.

Uamuzi ambao umepingwa vikali na asilimia 99% ya wasanii wa nchi hiyo kwa kusema iweje wao wapiganie tasnia hizo kwa shida kubwa kwa miaka mingi bila support ya serikali na Sasa serikali hiyo hiyo inakuja kibabe kupitisha Sheria zisizo rafiki bila hata kuwashirikisha wasanii wenyewe.

Sehemu ya andiko la serikali ya Nigeria ikionyesha ubabe fulani inasema.

“We urge the security agencies in the country to arrest Mr Peter Okoye for disrespecting our government and bringing it to a disrepute. If you cannot produce in Nigeria and hire Nigerians, then leave the industry. We must export Nigerian culture to the outside world through our music and videos”

Taasisi za Serikali zaagizwa kuandaa mpango wa mafunzo ya pamoja
Manji azidi kusota Gerezani, sasa aanza kupatiwa matibabu huko huko