Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amewataka wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la ‘Machinga’ kuondoka katika maeneo yanayotarajiwa kujengwa barabara za juu (Flyover) katika maeneo ya Ubungo.

Amesema kuwa lengo kuu ni kuwaondoa wafanyabiashara hao wadogo pasipokuwa na vurugu zozote na amewataka watu wengine kujifunza kutoka katika halmashauri hiyo jinsi ilivyoweza kukubaliana na wamachinga hao kuwaondoka katika maeneo hayo kupisha ujenzi huo pasipokutumia nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha, amewataka wamachinga kwenda kupanga biashara zao popote pale barabarani nje ya eneo la mradi, watakapo ona inafaa bila ya kubughuziwa na mtu yeyote, kufuatia kauli ya Rais Magufuli kuwa wamachinga wasisumbuliwe.

Hata hivyo, katika ziara hiyo, Jacob ameongozana na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo Bw.John Kayombo pamoja na maofisa kutoka ofisi za TANROANDS, Jeshi la Polisi, Wizara ya Ujenzi pamoja na Mkandarasi wa ‘Flyover’ Ubungo CCI- CCE

Video: Magufuli azuia ubomoaji wa nyumba 17,000 Dar
Nyama ya Punda yazidi kupanda bei, watumiaji walalamika