Klabu ya Barcelona imepaa kileleni mwa La Liga baada ya kuwachapa wakatalunya wenzao Espanyol kwa mabao 5-0 huku Lionel Messi akifunga mabao matatu.

Messi alitangulia kuipatia Barcelona bao la kwanza katika dakika ya 26 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ivan Rakitic ingawa bao hilo lilikuwa na utata ikionekana kama Messi aliotea kabla ya kufunga.

Dakika kumi kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Messi alipachika bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa  beki wa kushoto Jordi Alba.

Muargentina huyo alipiga hat-trick ya 38 akiwa na Barcelona baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Jordi Alba kwa mara nyingine kabla ya Gerard Pique na Luis Suarez kufunga mabao mengine mawili na kufanya mchezo huo kumalizika kwa mabao 5-0.

Katika mchezo huo mshambuliaji mpya wa Barcelona Ousmane Dembele aliyesajiliwa kutoa Borussia Dortmund aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya  Gerard Deulofeu na alitoa pasi kwa Luis Suarez iliyozaa goli la tano.

Ousmane Dembele aliingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Gerard Deulofeu

Kwa matokeo hayo Barcelona wanaongoza msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu waliyocheza huku wapinzani wake Real Madrid na Atletico Madrid wakisuluhu katiak michezo yao.

Video: Makonda azindua kiwanda cha wajasiliamali
IGP Sirro atoboa siri ya kukutana na viongozi wastaafu wa Polisi