Baba mzazi wa mchezaji Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta Pazi amesema kuwa anatarajia kutoa kitabu kinachozungumzia historia ya mwanae na siri ya kuwa mchezaji mkubwa duniani.
Mzee Samatta ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Polisi amesema kuwa ameamua kuandika kitabu hicho alichokipa jina “Huyu ndiye Samatta” kwa sababu watu wengi wanataka kumfahamu vizuri mwanae.
“Nimeamua kuandika kitabu kwa sababu napigiwa sana simu mpaka usiku wa manane… simu hadi kutoka Norway, Uingereza wanataka kujua habari za Samatta. Wanauliza huyu kijana mbona anacheza sana? Alianzaje?” Mzee Samatta ameiambia Nipe Tano ya TBC FM.
- Baada ya kutoa suluhu na Simba SC, Azam FC yaanika ratiba yake
- Messi apiga ‘Hat-trick’ Barcelona ikipaa kileleni
Mzee Samatta ambaye alikuwa mchezaji na mwalimu wa mpira kwenye timu za jeshi la polisi, amesema kitabu hicho kitatoka muda wowote kutoka sasa kikiwa na habari za Samatta ambazo nyingi hazijasikika .
Amesema baada ya kitabu hicho kinachozungumzia maisha ya mwanae, anatarajia kutoa kitabu kingine ambacho kitakuwa kinazungumzia maisha yake binafsi.