Shirikisho la soka nchini (TFF), limeongeza juhudi za kufundisha makocha wa mpira wa miguu hapa ili idadi ya walimu wa mpira wa miguu wanaopaswa kushiriki kwenye programu za maendeleo ya vijana za mikoa.
Hii ni katika kukidhi malengo ya TFF katika kusimamia maendeleo ya soka la vijana hapa nchini.
Kwa sasa, TFF kwa kushirikiana na mikoa ya Songwe, Lindi na Kigoma, zinaendeshwa kozi ngazi ya awali (Preliminary) na ngazi ya kati (Intermidiate).
Katika mkoa wa Songwe kozi ya ukocha zinazoendeshwa ni kozi ya awali Wilaya ya Songwe inayoendeshwa na Mkufunzi John Simkoko na kozi ya awali, wilaya ya Tunduma inaendeshwa na Mkufunzi George Mkisi.
Mkoani Lindi kozi ya awali ilianza Septemba 11, 2017 katika Wilaya ya Kilwa ikiendeshwa na Mkufunzi Michael Bundala na mkoani Kigoma kuna kozi mbili zinaendelea.
Moja ni ngazi ya awali inaendeshwa na Mkufunzi George Komba na kozi Ngazi ya Kati inaendeshwa na Mkufunzi Rogasian Kaijage.