Nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani LeBron James amewapongeza wachezaji wa ligi ya Marekani ‘NFL’ ambao wamefanya mgomo dhidi ya rais Donald Trump na kumtuhumu rais huyo wa Marekani kwa kutumia michezo ili kujaribu kugawanya watu.

Siku ya Ijumaa Trump alinukuliwa akisema kwamba wachezaji wa ligi ya NFL ambao walishindwa kusimama wakati wa wimbo wa taifa walifaa kufutwa kazi au kusimamishwa kwa muda.

Baada ya Tramp kusema maneno hayo wikendi iliopita katika mchezo wa ligi ya NFL baina ya timu za Baltimore Ravens na Jacksonville Jaguars, wachezaji walijibu kwa kupiga goti moja chini huku wengine wakiamua kusalia katika chumba cha maandilizi wakati wimbo wa taifa wa Marekani ukipigwa.

LeBron James aliwapongeza wachezaji hao na kusema kuwa hatamruhusu mtu mmoja licha ya uwezo wake kutumia michezo kama kigezo cha kuwagawanya wamarekani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye anaichezea Cleveland Cavaliers alimfanyia kampeni Hillary Clinton, ambaye alikuwa mpinzani wa Trump wakati wa kinyang’anyiro cha urais mwaka 2016.

 

 

Kadinda amlipua Wema Sepetu ataja udhaifu wake mkubwa
Maalim Seif aongoza jopo la viongozi Kenya kwa Lissu