Leo Septemba 26, 2017, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Antipas Lissu ambaye alipigwa risasi.

Mwenyekiti wa kamati ya  muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe.Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe.Tundu Lissu ‘’. Amesema Mtatiro.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zai

 

LeBron James: Sitakubali Trump kutumia michezo kutugawanya
Man Utd wajiandaa kwa Paulo Dybala