Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa soko la filamu za kitanzania linazidi kukua kadri siku zinavyozidi kusonga mbele huku ushindani ukiongezeka.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya ‘Bei Kali’ iliyoigizwa na msanii Simon Mwakipagata maarufu kwa jina la ‘Rado’ ambapo amewataka watanzania kununua filamu hizo.
“Kwa sasa soko linazidi kukua kadri muda unavyozidi kusonga mbele, hivyo jitahidini wasanii wetu kwani hii fursa mojawapo ya ajira, mkifanya vizuri itaweza kuwakwamua,”amesema Dkt. Mwakyembe
Hata hivyo, amewapongeza wasanii walioshiriki katika filamu hiyo huku akisema kila mmoja ameitendea haki sehemu yake aliyoiigiza.