Baada ya ukimya wa muda mrefu nyota wa filamu nchini Simon Mwakipagata maarufu kama Rado ametoa filamu yake mpya inayoitwa ‘Bei kali’.

Akiongea wakati hafla ya kutambulisha Filamu hiyo katika ukumbi wa Mlimani City Rado amesema filamu hiyo ilitakiwa kuwa imefanyika miaka minne iliyopita lakini tatizo lilikuwa ni bajeti. Rado amesema alitaka kumshirikisha Wema Sepetu na msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ambaye alihitaji kiasi cha milioni 100 kiasi ambacho yeye binasfi asingeweza kutoa.

Rado ameongeza kuwa amechukua maoni ya mashabiki ambao wamekuwa wakilalamikia ubora wa filamu za Tanzania na kuamua kufanya filamu nzuri inayokidhi viwango.

Tazama mahojiano yake hapa chini;

Azam FC kupimana na Ngorongoro Heroes
Video: Familia ya Lissu yatoa msimamo wake